Toptube Video Search Engine



Title:Mkasi | SO9E06 with Aunty Ezekiel
Duration:27:02
Viewed:269,902
Published:28-07-2014
Source:Youtube

Mwaka 1986, mnamo tarehe 28 Oktoba, anga la sanaa Tanzania liliongeza Nyota ingine. Si Mwingine bali ni Aunty Ezekiel Greyson. Kwa wale wakongwe watamkumbuka Ezekiel Greyson aka Jujuman, mmoja wa wanasoka maarufu miaka ya 1970 na 1980, naye ndie baba Mzazi wa Nyota wetu. Ambacho hatukujua ni kuwa leo hii, huyu angekuja kuwa mmoja kati ya kivutio kikubwa kwenye tasnia ya Uigizaji Filamu nchini na hata pale popote Kiswahili kinapofika. Akiwa mtoto wa pekee kike kwa Baba yake, ilizua tafrani kwa mashangazi zake, kila mmoja akitaka mtoto aitwe jina lake, kuondoa ugomvi, ndipo alipopewa jina la "Aunty" kuwakilisha Mashangazi zake wote bila ubaguzi. Maisha yake baada ya Elimu za awali yaliingiliwa na ukakasi pale alipokosakosa kuolewa bila yeye kuridhia, hata hivyo baada ya kuingia mjini na kuhangaika alivyoweza hatimae alifanikiwa kuendelea na masomo kidato cha nne na kompyuta. Kuingia katika Sanaa ya Uigizaji kulianza pale aliposhiri Miss Mwanza mnamo mwaka 2006, wakati akiwa katikati ya shughuli ya uigizaji wa filamu ya "Miss Bongo" iliyoongozwa na William Mtitu. Kutokufanikiwa katika mashindano hayo ya Miss Tanzania kulimfanya afanye uchaguzi wa kubaki katika fani ya uigizaji aliyoendelea nayo mpaka hii leo. Upande wa mahusiano ya Kimapenzi, Aunty alikutana na PDG maarufu Jijini Jack Pemba, ambae walifunga ndoa mwaka 2007, na pamoja na mifarakano ya hapa na pale ndani ya ndoa, zaidi kwa sababu ya wivu wa penzi, Aunty alifanikiwa kupata ujauzito, ingawa haikuwa rizki kwani ilipofika miezi 7 alijifungua na mtoto kufariki. Mambo hayakwenda kama ilivyotarajiwa hatimae akatengana na Jack. Kwa sasa ameolewa tena na anaendeleza fani yake.....ingawa la muhimu zaidi....ameonekana kuwa karibu sana na Wema Sepetu, mshindi wa Shindano la Unyange la 2006, na pia rafiki wa kiume wa Wema, Diamond na wengineo! Mastaajabu hayaishi, utamsikia akiongea mengi na Mkasi TV, na zaidi, kupata undani wa nini tutegemee toka kwake. L•O•V•E Follow MkasiTV on Facebook : http://facebook.com/MkasiTV Twitter : @MkasiTV Instagram @MkasiTV



SHARE TO YOUR FRIENDS


Download Server 1


DOWNLOAD MP4

Download Server 2


DOWNLOAD MP4

Alternative Download :